Informações:
Sinopse
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episódios
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya maneno "MBEUZI, MNYWANYWA NA MACHAGU.”
12/06/2025 Duração: 54sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno "MBEUZI, MNYWANYWA NA MACHAGU.”
-
12 JUNI 2025
12/06/2025 Duração: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupinga utumikishaji wa watoto ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO, linasema maudhui ni Maendeleo yako dhahiri, lakini bado kuna mengi ya kufanya: Hebu tuongeze kasi. Tunakupeleka nchini Tanzania kumulika harakati za kuwaepusha watoto kutumikishwa.Watu waliolazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita, ukatili na mateso duniani kote imefikia kiwango cha juu kisichovumilika, hasa wakati huu ambapo ufadhili wa misaada ya kibinadamu unapungua kwa kasi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa leo kuhusu mwelekeo wa Ulimwengu, kufikia mwisho wa Aprili mwaka huu, kulikuwa na watu milioni 122.1 waliolazimika kuhama kwa nguvu, ikilinganishwa na watu milioni 120 mwaka uliopita katika kipindi kama hicho.Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto, utafiti uliofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kazi duniani, ILO na la kuhudumia Watoto UNICEF
-
Masuala ya watu wenye ulemavu ni lazima yapewe nafasi kimataifa: Jakeel D. Abdullah
11/06/2025 Duração: 01minKatika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18, kinaendelea na mwaka huu, mada kuu ni kuongeza uelewa wa haki na mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya kijamii. Miongoni mwa washiriki ni ya kijana kutoka Louisiana, hapa Marekani. Je amesema nini? Flora Nducha na taarifa zaidi
-
Akili Mnemba (AI) au teknolojia inaweza kuwasaidia watu wenye ulemavu – Bongani Simphiwe Makama
11/06/2025 Duração: 03minKikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu – COSP18 – kinaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ikiangazia juhudi za kimataifa za kuhakikisha usawa na ujumuishaji kwa watu wenye ulemavu. Miongoni mwa washiriki ni Bongani Simphiwe Makama mwakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka Ufalme wa Eswatini, ambaye amepata nafasi ya kuzungumza na Idhaa ya Kiswahili kuhusu uzoefu wake, yale aliyojifunza, na changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu nchini kwake. Sharon Jebichii na Makala zaidi.
-
11 JUNI 2025
11/06/2025 Duração: 09minHii leo jaridani tunaangazia ajali mbayá ya meli katika pwani ya Djibouti lililokuwa linabeba wahamiaji wengi. Pia tunasalia hapa makao makuu ambapo Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18. Mashinani tutakwenda nchini DRC.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM) kwa ushirikiano wa karibu na mamlaka za Djibouti, linaongeza juhudi zake za kibinadamu kufuatia tukio la kusikitisha lililotokea pwani ya Djibouti ambapo takriban wahamiaji wanane walikufa maji na wengine 22 hawajulikani walipo.Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18, kinaendelea na mwaka huu, mada kuu ni kuongeza uelewa wa haki na mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya kijamii. Miongoni mwa washiriki ni ya kijana kutoka Louisiana, hapa Marekani.Makala tutasalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani ambapo Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu
-
IOM yachukua hatua za dharura baada ya wahamiaji kufa maji katika pwani ya Djibouti
11/06/2025 Duração: 01minShirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM) kwa ushirikiano wa karibu na mamlaka za Djibouti, linaongeza juhudi zake za kibinadamu kufuatia tukio la kusikitisha lililotokea pwani ya Djibouti ambapo takriban wahamiaji wanane walikufa maji na wengine 22 hawajulikani walipo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
-
10 JUNI 2023
10/06/2025 Duração: 10minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika ukanda wa Gaza, huko mashariki ya Kati kwenye eneo la Palestina lialokaliwa kimabavu na Israeli ambapo vinazidi kuibua changamoto mpya kila uchao.Changamoto ya uzazi duniani si kuhusu watu kukataa kuwa wazazi ni kuhusu kunyimwa fursa ya kuchagua kuwa mzazi imesema ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA iliyotolewa leo na kuonesha kuwa kuwa matatizo ya kiuchumi, ukosefu wa usawa wa kijinsia, na hofu kuhusu maisha ya baadaye vinawazuia mamilioni ya watu kupata familia wanazotamani.Tishio la baa la njaa linaendelea kuiandama Sudan iliyoharibiwa vibaya na vita, limeonya leo Shirika laUmoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, likitoa wito wa dharura kwa jamii ya kimataifa kusaidia kukidhi mahitaji yanayoongezeka na kuzuia maafa zaidi ya kibinadamu.Kwa mara ya kwanza dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya Mazungumzo baina ya Ustaarabu tofauti yenye lengo la kuchagiza amani, maelewano na mshikamano k
-
UNEP inashirikiana na taifa la Tanzania kupambana na taka za plastiki - Clara Makenya
09/06/2025 Duração: 06minMkutano wa tatu wa Umoja wa Mataiifa kuhusu Bahari UNOC3 ukiendelea mjini Nice, Ufaranzsa, tunakuletea mahojiano kati ya Nafisa Didi afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam na Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, wakimulika mchango wa UNEP katika kuzisaidia nchi kupambana na taka za plastiki ambayo ni mada kuu ya mkutano wa UNOC3.
-
Mustakabali wa bahari u mikononi mwetu sisi tunaoiharibu - UN
09/06/2025 Duração: 02minMkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo António Guterres bila kumung’unya maneno ameelezea bayana jinsi binadamu anavyozidi kuhatarisha ustawi wa bahari lakini akionesha matumaini ya hali bora ya bahari iwapo hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya binadamu na viumbe vya baharini. Assumpta Massoi amefuatilia na kuandaa taarifa hii.
-
09 JUNI 2025
09/06/2025 Duração: 11minHii leo jaridani tunaangazia Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa, na masuala ya baharini ikiwa ni pamoja na uvuvi nchini Sao Tome, umuhimu wa kutunza mazingira nchini Kenya na uondoaji wa taka za plastiki Tanzania.Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo António Guterres bila kumung’unya maneno ameelezea bayana jinsi binadamu anavyozidi kuhatarisha ustawi wa bahari lakini akionesha matumaini ya hali bora ya bahari iwapo hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya binadamu na viumbe vya baharini.Nchini São Tomé na Príncipe, nchi ya visiwa viwili vidogo huko Afrika ya Kati, mpango wa FISH4ACP unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO unalenga kusaidia wavuvi na wauzaji samaki hasa wanawake na vijana kuongeza kipato na manufaa ya kijamii kwa njia endelevu huku wakipunguza athari mbaya kwa makazi ya asili na viumbe wa baharini. Paola Afè Do Espiritu Afonso ni miongon
-
São Tomé na Príncipe: Viumbe wa bahari, samaki, ni chanzo cha mapato, kuinua jamii na kuondoa umaskini
09/06/2025 Duração: 02minNchini São Tomé na Príncipe, nchi ya visiwa viwili vidogo huko Afrika ya Kati, mpango wa FISH4ACP unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO unalenga kusaidia wavuvi na wauzaji samaki hasa wanawake na vijana kuongeza kipato na manufaa ya kijamii kwa njia endelevu huku wakipunguza athari mbaya kwa makazi ya asili na viumbe wa baharini. Paola Afè Do Espiritu Afonso ni miongoni mwa wanawake wanaonufaika, Sharon Jebichi na maelezo zaidi.
-
Jifunze Kiswahili: maana ya neno KIHEREHERE
05/06/2025 Duração: 45sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno KIHEREHERE.
-
05 JUNI 2025
05/06/2025 Duração: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo leo ikiwa ni siku ya mazingira duniani mwaka ikibeba maudhui “Tokomeza taka za Plastiki,” tunakwenda Tanzania kumsikia Clara Makenya, Mkua wa UNEP nchini humo na afisa mawasiliano wa shirika hilo kwa ajili ya Namibia akizungumza kuhusu changamoto ya taka za plastiki Tanzania na nini kifanyike kuzitokomeza.Naanzia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani ambapo leo kumefanyika tukio maalum la kukumbuka na kuenzi watumishi 168 wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha wakitekeleza majukumu yao ya ulinzi wa amani, haki, na usaidizi, Mishumaa iliwashwa na kisha walitajwa majina yao mmoja baada ya mwingine akiwemo Nats.. mlinda amani wa UN kutoka Tanzania. Wanafamilia walipokea tuzo maalum za kutambua mchango wao.Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mazingira, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka hatua za dharura kutokomeza janga la uchafuzi utokanao na taka za plastiki, akilitaja kama “janga” linaloikaba dunia na kutishia afya ya binad
-
Uwekezaji sahihi ni ule unaoanzia kwa wananchi na si ngazi ya juu - Madina
04/06/2025 Duração: 02minMkutano wa siku mbili kuhusu Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya dunia endelevu umekunja jamvi huko Hamburg nchini Ujerumani ambako Balozi wa Mabadiliok ya Tabianchi wa Vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania, Madina Jubilate Kimaro ameshiriki.
-
04 JUNI 2025
04/06/2025 Duração: 09minHii leo jaridani tunaangazia haki za jamii za Ogiek nchini Kenya, na masuala ya baharí na tabianchi. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Mtaalamu wa UN ataka kusitishwa mara moja kwa uwekaji mipaka unaotishia haki za Waogiek Kenya. Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa ameitaka Serikali ya Kenya kusitisha mara moja shughuli za uwekaji mipaka katika Msitu wa Mau Mashariki nchini humo, akisema kuwa unakiuka haki za jamii ya asili ya Waogiek na kupuuza maamuzi ya lazima ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR).Mkutano wa siku mbili kuhusu Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya dunia endelevu umekunja jamvi huko Hamburg nchini Ujerumani ambako Balozi wa Mabadiliok ya Tabianchi wa Vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania, Madina Jubilate Kimaro ameshiriki. Akiwa huko Hamburg nimemuuliza Madina ni kipi amejulisha washiriki wenzake kuwa kinapaswa kufanyika ili dunia iwe endelevu?.Makala, katika
-
Kuelekea Mkutano wa Bahari UNOC3, UNEP yatoa wito wa hatua za kukabili taka za plastiki
04/06/2025 Duração: 03minKatika kuelekea Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari UNOC3, utakaofanyika mjini Nice, Ufaransa kuanzia tarehe 9 hadi 13 Juni 2025, Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na madhubuti kukabiliana na changamoto ya uchafuzi wa bahari, hasa wa taka za plastiki. Akizungumza na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo UNIC jijini Dar es Salaam, Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, alisisitiza umuhimu wa kushughulikia kwa haraka tatizo la taka za plastiki ambazo nyingi hutokea nchi kavu na kuishia baharini.
-
Mtaalamu wa UN ataka kusitishwa mara moja kwa uwekaji mipaka unaotishia haki za Waogiek nchini Kenya
04/06/2025 Duração: 01minMtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa ameitaka Serikali ya Kenya kusitisha mara moja shughuli za uwekaji mipaka katika Msitu wa Mau Mashariki nchini humo, akisema kuwa unakiuka haki za jamii ya asili ya Waogiek na kupuuza uamuzi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR). Anold Kayanda na maelezo zaidi.
-
03 JUNI 2025
03/06/2025 Duração: 10minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kinainayomulika kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi katika kaunti kama Kajiado, Kenya, ambayo jamii hukumbwa na hali ya ukame na mazingira magumu, mabadiliko chanya yanaonekana.Mustakabali wa mzingiro wa Israeli kwenye eneo la Palestina la Gaza inalokalia kimabavu ukiendelea kukumbwa na sintofahamu, wanawake na wasichana wamesimulia adha ya ukosefu taulo za kike wakati wanapokuwa kwenye hedhi huku upatikanaji wa maji ukiwa ni wa taabu.Idadi ya wakazi wa nchi zenye maendeleo duni, LDCs na zile za visiwa vidogo, SIDS wanaopata huduma zilizoboreshwa au za kisasa za maonyo ya mapema kabla ya majanga imefikia takribani milioni 400 na hii ni kutokana na programu ya CREWS iliyoanzishwa mwaka 2015 na shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO.Rebecca Kalonji, al maaruf Sista Becky, mwimbaji chipukizi wa mtindo wa kufokafoka kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hii leo ametangazwa kuwa Muungano Mkono wa Ngazi ya Juu wa masuala ya lishe na ulaji wenye a
-
Shirika la kiraia lawezesha vijana wa kike kujiajiri badala ya kutumbukia kwenye umaskini
02/06/2025 Duração: 03minNchini Tanzania ugumu wa maisha na kukabiliwa na vishawishi, umewapa fikra mpya vijana wa kike mkoani Morogoro, mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambao sasa wanajimudu kiuchumi, kwa kuanzisha biashara na shughuli za ujasiriamali. Wanasongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs hususan namba 8 la ajira zenye staha, nan amba 1 la kutokomeza umaskini. Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania Kids Time FM amewatembelea vijana hao na kuandaa makala hii.
-
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ashutumu mashambulizi dhidi ya Wapalestina wanaotafuta msaada
02/06/2025 Duração: 01minKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameeleza kughadhabishwa kufuatia kusambuliwa, kujeruhiwa na kuuawa kwa Wapalestina walipokuwa wakijaribu kupata msaada wa kibinadamu huko Gaza jana Jumapili, Juni Mosi. Selina Jerobon na taarifa zaidi.