Siha Njema

Uhusiano wa karibu kati ya matatizo ya tezi koo na afya yako ya akili

Informações:

Sinopse

Matatizo ya tezi koo yanaweza kujidhirisha kwa  dalili kama vile msongo wa mawazo,kukosa usingizi,kiwewe na mtu kukosa ari ya chochote maishani Katika makala haya ,tunamtambulisha Daktari Violet Oketch anayesimamia kitengo cha afya ya akili katika hospitali  kuu ya rufaa nchini Kenya ya Kenyatta. Daktari Violet anafafanua ufungumano kati ya matatizo ya tezi koo na matatizo ya afya ya akili. Aidha afisa mkuu mtendaji wa kikundi cha kuhamasisha kuhusu matatizo ya tezi koo,Thyroid  Disease Awareness Kenya Foundation ,TDAK,  Sarah Katulle anaelezea umuhimu wa wagonjwa kuwa kwenye kundi ambapo wanaweza kushirikishana kuhusu mbinu mbadala ya kuishi na matatizo hayo kando na matibabu. Kundi hilo linawasaidia wagonjwa kupata matibabu kwa urahisi kwa kushirikiana na madaktari bingwa ,mahabara maalum na dawa sahihi. Aidha TDAK ili kuwasaidia wagonjwa hao kuishi maisha ya kawaida wakiwa kazini ,inawaandikia barua ambazo zinawasilishwa kwa maajiri kutambua hali halisi ya wagonjwa na mahitaji yao.