Habari Za Un

02 JUNI 2025

Informações:

Sinopse

Hii leo jaridani tunaangazia haki za kibidamu katika ukanda wa Gaza, na hali ya misaada ya kibinadamu huko huko Gaza. Makala yunakwenda nchini Tanzania kusikia harakati za kusaidia vijana wa kike, na mashinani tunakupeleka nchini Uganda kusikia kuhusu mradi wa mlo shuleni.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameeleza kughadhabishwa kufuatia kusambuliwa, kujeruhiwa na kuuawa kwa Wapalestina walipokuwa wakijaribu kupata msaada wa kibinadamu huko Gaza jana Jumapili, Juni Mosi.Maisha ya raia wa Gaza ambao karibu wote ni wakimbizi wa ndani yanazidi kuwa mtihani usio na majawabu kila uchao kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa. Mateso wanayopitia nis awa na kuishi jrehanamu, wengi wamekata tamaa na wanaona bora kufa kuliko kuishi katika hali hiyo. Flora Nducha akusimulia madhila ya mmoja wa wakimbizi hao wa ndani Moamen Abu Asr na mkewe Zeinat..  Makala inakupeleka nchini Tanzania kusikia harakati za kunasua vijana wa kike kutoka vishawishi vinavyoweza kuwatumbukiza kwenye lindi