Habari Za Un
20 MEI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 0:12:20
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika wafugaji wa nyuki nchini Tanzania leo ikiwa ni siku ya nyuki duniani iliyopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 20 Desemba mwaka 2017 kupitia azimio namba A/72/211.Baada ya miaka mitatu ya majadiliano, leo katika Mkutano wa Kimataifa wa Afya unaoendelea Geneva, Uswisi, nchi zimepitisha rasmi makubaliano ya kihistoria ya kuzuia, kujiandaa, na kukabiliana vyema na majanga ya magonjwa kwa siku zijazo. Taratibu zote zitakapopitishwa na angalau nchi 60, mkataba utaanza kutumika rasmi mwakani.Kutokana na mamlaka za Israeli kulegeza kwa muda mzingiro uliodumu kwa wiki 11, angalau sasa matumaini kidogo yamerejea Gaza, yameeleza leo mashirika ya Umoja wa Mataifa. Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya dharura, OCHA, Jens Laerke amesema tayari wamepata ruhusa ya kuyavusha malori matano yaliyokuwa yamezuiliwa jana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limetahadharisha leo kwamba bila ufadhili zaidi, huenda kati