Habari Za Un

22 APRILI 2025

Informações:

Sinopse

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inatupeleka Msasani nchini Tanzania kusikia namna vijana na serikali wanavyolinda Mama Dunia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari ujumbe wa Katibu Mkuu, watoto kulinda mazingira DRC, na kifo cha Papa Francis.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya Mama Dunia, ikilenga kuchagiza hatua ya kuhifadhi sayari dunia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametumia neno ‘homa’ kuwa inakumba dunia hivi sasa kutokana na viwango vya joto vinavyoongezeka kila mwaka. Hata hivyo amesema majawabu ya kutibu homa hiyo yapo ikiwemo kutumia nishati rejelezi ambayo ni rahisi, ina afya na salama kuliko nishati kisukuku.Huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kando ya mapigano yanayotikisa eneo la mashariki mwa nchi, watoto wamechukua hatua kulinda sayari dunia kwa kuhifadhi misitu kwenye taifa hilo ambako ukataji miti kiholela umefurutu ada.Kufuatia kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis hapo jana Jumatatu, ambaye maziko yake yamepangwa kufanyika