Habari Za Un
24 APRILI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 0:11:35
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Chata ya Umoja wa Mataifa inayolenga kusongesha amani, maendeleo, urafiki na haki za binadamu. Je, wajumbe wa Umoja wa Mataifa hufanya nini? Assumpta Massoi amezungumza na mmjoa wao Balozi Yabesh Monari wa Kenya, lakini kwanza ni muhtasari wa habari na ufafanuzi wa maneno.Mratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Matthias Schmale, amelaani vikali shambulio jipya la Urusi dhidi Ukraine lililosababisha vifo na majeruhi kwa raia, wakiwemo watoto na mwanamke mjamzito. Bwana Schmale amesema shambulio hilo la usiku wa kuamkia leo katika maeneo ya makazi jijini Kyiv na maeneo ya jirani ni ukiukaji wa kutisha wa sheria za kimataifa za kibinadamu na kwamba matumizi haya ya nguvu yasiyo na maana lazima yakome.Wiki ya Chanjo Duniani ikiwaimeanza leo, mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani, WHO, na la kuhudumia Watoto, UNICEF, na Ubia wa chanjo duniani, Gavi wametoa onyo kwamba milipuko ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo inaon