Habari Za Un

09 APRILI 2025

Informações:

Sinopse

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan, na haki za binadamu na watu kutoweka kwa wingi nchini Sudan. Makala inatupeleka nchini Kenya na Mashinani tunakwenda Gaza, kulikoni?Nchini Sudan Kusini, familia zilizo kwenye hali duni katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ziko katika hali tete sana huku mapigano yakizidi kuongezeka na njaa ikikaribia kufikia viwango vya juu kabisa, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).Wakati hofu ikiendelea kuhusu watu kutoweka kwa wingi nchini Sudan, Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa aliyeteuliwa na Ofisi ya Haki za Binadamu OHCHR anayehusika na haki za binadamu nchini humo Radhouane Nouicer ametoa wito wa dharura kuhusu hali ya raia waliokwama katika vita kubwa nchini humo.Katika inatupeleka nchini Kenya kufuatilia simulizi ya Shalyne Kaputa, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 16 kutoka kaunti ya Turkana ambaye tofauti na shangazi yake ambaye hakuweza kuendelea na elimu  ya