Habari Za Un
10 APRILI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 0:09:59
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Idhaa hii inazungumza na Mwenyekiti wa Tanzania Women Ecocomic Empowerment Network (TAWEN), ambaye pia ni mchumi mbobezi Bi. Janet Zebedayo Mbene. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki.Shukran Anold na leo tunaanzia huko Geneva Uswisi ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limetoa muongozo wake wa kwanza duniani wa kutambua, kutoa matibabu kwa haraka na matibabu ya muda mrefu kwa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.Nchini Chad katika mpaka wake na Sudan ambako Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi ametembelea na kuzungumza na wakimbizi wa Sudan pamoja na kujionea hali zao wakati huu ambapo wamepunguza kutoa chakula, malazi , maji na dawa na kauli yake ikawa moja tu, “Ninatoa wito kwa wafadhili, tafadhali msipunguze msaada kwa wathirika wa vita vya Sudan.”.Taarifa ya pamoja ya mashirika ya kibinadamu inayotolewa kila baada ya wiki mbili imeeleza kuhusu hali katika Ukanda wa Gaza