Habari Za Un

11 APRILI 2025

Informações:

Sinopse

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya watoto nchini DR Congo, na masuala y awanawake nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Kenya kuangazia harakati za vijana za kusongesha Ajenda2030, na mashinani tunasalia huko huko kumulika misaada kwa wakimbizi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limeripoti kwamba huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kila nusu saa takribani mtoto mmoja anaripotiwa kubakwa huku ghasia zikiendelea katikati ya janga linalozidi kukua la ufadhili finyu wa kifedha.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN WOMEN nchini Tanzania chini ya ufadhili kutoka Muungano wa Ulaya wanashirikiana na jeshi la polisi kuendesha mradi huko visiwani Zanzibar wa kukomesha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana na tayari manufaa ya mradi huo yameanza kuonekana.Makala leo inatupeleka Nairobi Kenya kwa Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi akizungumza na Winifred Njiru mwanafunzi wa chuo kikuu fani ya uhakiki au qua