Habari Za Un

Tume huru ya UN ya kusaka ukweli kuhusu Sudan imelaani vikali mauaji ya watu zaidi ya 100

Informações:

Sinopse

Vita ya sasa ya Sudan ikielekea kuingia mwaka wa tatu, Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya kusaka ukweli kuhusu Sudan imelaani vikali mauaji ya watu zaidi ya 100 yaliyotokea wikiendi hii katika kambi za wakimbizi wa ndani Darfur, ikionya kwamba hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Anold Kayanda na taarifa zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Shukrani LeahTangu kuanza kwa vita kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na kikosi cha waasi cha RSF mnamo tarehe 15 Aprili mwaka 2023, maelfu ya watu wamepoteza maisha, huku mamilioni wakikumbwa na njaa, ubakaji, na ufurushwaji. Kambi kama ya Zamzam, yenye wakazi zaidi ya laki saba – nusu yao wakiwa watoto – zinaripotiwa kuzingirwa, wakazi wake wakikosa chakula, dawa, na maji, imeeleza Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya kusaka ukweli kuhusu Sudan.Mwenyekiti wa tume hiyo, Mohamed Chande Othman, ananukuliwa akisema, “Dunia imeshuhudia miaka miwili ya mzozo usio na huruma ambao umewanasa mamilioni ya raia katika mazingira ya kutisha, wakiwekwa katika hali ya ukatili bila matumaini ya mwisho.”Kwa mu