Habari Za Un
16 APRILI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 0:09:57
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika masuala ya afya hususan harakati za kukabiliana na majanga yajayo ya afya; wakimbizi huko Zambia ambako sera jumuishi zimewajengea uwezo; Jukwaa la vijana na mchango wa sanaa kwenye usawa na utengamano. Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo huko mjini Geneva, Uswisi, nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi ujao wa Mei. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi.Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola. Limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, likiongeza kwamba kwa kuzingatia sera jumuishi ya Zambia,