Habari Za Un

Uhaba wa fedha watishia ukarimu wa Zambia kwa wakimbizi - UNHCR

Informações:

Sinopse

Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, ambalo limesema kwa kuzingatia sera yake jumuishi, nchi hiyo inakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. Flora Nducha na taarifa zaidi  Shirika hilo la wakimbizi limesema katika makazi kama Mayukwayukwa na Maheba ambayo ni moja ya kambi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Zambia familia za wakimbizi zilizolazimika kukimbia makwao zinajumuishwa ili ziweze kujikimu na kuishi kwa utangamano na wenyeji wanaowahifadhi. Moulid Hujale, ni afisa habari msaidizi wa UNHCR anasema “Selikali ya Zambia inajumuisha wakimbizi katika huduma za kitaifa kama vile elimu na hata programu za msaada wa kilimo  ili kuongeza uzalishaji” Amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo Zambia imeone