Gurudumu La Uchumi
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editora: Podcast
- Duração: 3:58:40
- Mais informações
Informações:
Sinopse
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Episódios
-
Wataalamu waonya kuhusu pengo la walionacho na wasionacho
22/01/2025 Duração: 09minMsikilizaji ripoti mpya ya shirika la kupambana na umasikini Oxfam, inaonesha kuwa utajiri wa mabilionea uliongezeka mara tatu zaidi katika mwaka uliopita, ikiwa ni zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2023.Katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tumezungumza Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara, kuangazia kwa kina ripoti hii na athari ya kuendelea kushuhudiwa kwa pengo la matajiri na masikini.
-
Nchini Kenya Vijana wa mitaa duni wakumbatia Teknolojia ya biashara ndogo ndogo
15/01/2025 Duração: 09minTeknolojia bunifu ya biashara ndogo ndogo imekuwa ikijulikana kuwa ya watu waliojiweza katika jamiii kutokana na gharama yake ,hali ambayo inawafungia nje watu hasa vijana kutoka maeneo duni na vijijini hivyo kukosa kuimarika kibiashara na kiuchumi kupitia teknolojia hizo .Lakini hata hivyo vijana pamoja na mashirika mbalimbali mtaa wakibera jijini Nairobi Kenya wapata fursa ya mafunzo na kuimarika kibiashara
-
Sehemu ya II: Umuhimu wa kuwa na nidhamu ya kuweka akiba ya fedha
08/01/2025 Duração: 10minHivi leo ni sehemu ya pili ya makala ya Gurudumu la Uchumi, hasa tunapouanza mwaka 2025 tunaenda kujadili kuhusu nidhamu ya kuweka akiba ya fedha, ufanye nini kuongeza kipato, unatumiaje fedha ulizonazo kuwekeza ? Haya ni baadhi ya mambo ambayo tutaenda kuyatazama kwenye makala ya juma hili. Tutakuwa na Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
-
Sehemu ya I: Kwanini ni muhimu kuwa na nidhamu ya kuweka akiba ya fedha
01/01/2025 Duração: 09minHeri ya mwaka mpya 2025 msikilizaji wa RFI Kiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu na hasa makala ya Gurudumu la Uchumi, ni imani yetu kuwa nyote mbuheri wa afya. Makala ya Gurudumu la Uchumi, tutajadili kuhusu nidhamu ya kuweka akiba ya fedha. Kuzungumzia hili msikilizaji kwenye line ya simu nimemualika Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.