Informações:
Sinopse
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Episódios
-
CAF: Droo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada yakamilika
23/11/2024 Duração: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa droo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada 2024, fainali ya klabu bingwa Afrika kwa kina dada, nini maana ya Tanzania na Uganda kuwakilisha CECAFA kwenye AFCON 2024, mechi za kufuzu ligi ya Afrika ya Basketboli na michuano ya kufuzu Mashindano ya Afrika ya Basketboli, ligi za ukanda na ulaya Pep Guardiola atia saini mkataba mpya klabuni Man City.
-
AFCON 2025: Uganda yafuzu fainali za mwaka kesho huku Kenya, Ghana zikitupwa nje
16/11/2024 Duração: 23minTuliyoyazungumzia ni pamoja na upekee wa klabu ya voliboli nchini Kenya ya Trailblazers, uchaguzi wa FKF nchini Kenya umeanza, mabadiliko ya makocha klabuni Yanga, timu ya taifa ya Kenya ya walemavu ya soka yamaliza nafasi ya nne Kombe la Dunia, uchambuzi wa michuano ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2025 na pigano la Jake Paul dhidi ya Mike Tyson
-
CAF: Ligi ya klabu bingwa barani Afrika 2024 kwa kina dada yaanza nchini Morocco
09/11/2024 Duração: 23minTumeangazia klabu ya Chaux Sport kutoka DRC kubanduliwa kwenye mechi za kufuzu Ligi ya Basketboli Afrika 2024, masaibu ya Yanga SC nchini Tanzania, uchaguzi wa FKF nchini Kenya, mashindano ya kuendesha baiskeli Afrika kwa kina dada nchini Burundi, kifo cha rais wa soka nchini Algeria, matokeo na uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya na fainali ya tenisi kwenye mashindano ya WTA
-
Senegal kuwa mwenyeji wa mashindano ya Olimpiki ya kwanza kabisa Afrika, 2026
02/11/2024 Duração: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na bodi mpya ya uchaguzi wa shirikisho la soka nchini DRC, waziri wa michezo nchini Tanzania Damas Ndumbaro abainisha viwanja 20 kwa ajili ya AFCON 2027, timu ya REG nchini Rwanda yafuzu Ligi ya Basketboli Afrika 2024 kwa kina dada, mechi za kufuzu CHAN 2025, hatma ya kocha wa Rwanda Torsten Spittler, Senegal kuandaa michezo ya Olimpiki ya kwanza barani Afrika ya chipukizi mwaka 2026, kocha mpya wa Man Utd, mashindano ya Paris Masters na Brazilian GP Afrika inatarajia michezo ya kwanza ya Olimpiki ya vijana itakayoandaliwa barani Afrika mwaka 2026, jijini Dakar, mji mkuu wa Senegal.Michezo hiyo imepangwa kufanyika kati ya Oktoba 31 na Novemba 13, 2026, tukio ambalo litaleta pamoja wanariadha bora zaidi ulimwenguni kushiriki katika michezo 35 tofauti kwa siku 14.Tamasha la Dakar en Jeux (Dakar in Games) lilipangwa awali kwa kipindi cha Dakar 2022, katika miji mitatu ya mwenyeji wa Dakar, Diamniadio, na Saly.Tangu wakati huo, Dakar en Jeux imekuwa sherehe ya kila mwaka ya michezo na ut