Informações:
Sinopse
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episódios
-
Hali halisi ya Malaria barani Afrika wakati huu ufadhili ukiendelea kushuka
10/03/2025 Duração: 10minSerikali za Afrika zitalazimika kuchangia ufadhili wa mipango ya kupambana na Malaria kufidia pengo kubwa la ufadhili Muungano wa viongozi wa Afrika wa kupambana na Malaria ,Africa Leaders Malaria Alliance unasema Afrika inahitaji dola bilioni 5 nukta nane mwaka huu wa kifedha hadi 2026.Hali hii pia imechangiwa na Marekani kukata ufadhili wa misaada kwa nchi za kigeni
-
Kukata kiu ya jamii zinazoishi mpaka wa Kenya na Somalia ,waathiriwa wa mgogoro
25/02/2025 Duração: 08minMamia ya wakaazi wa kaskazini mashariki mwa Kenya maeneo yanayopakana na Somalia na waathiriwa wakubwa wa mzozo wa Somalia hawajakuwa na maji masafi , hali hiyo ikizidisha mgogoro wa kijamii ndani ya jamii hii ya wafugaji wanaotokea upande wa Kenya na upande mwingine wa Somalia. Kukabili hali hii ,kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu , International Committee of the Red cross ,ICRC , shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya ,Kenya Red Cross,KRC katika mkakati wa kuleta amani na ustawi imekuwa ikifanya miradi ya kuwapa wakazi maji .Carol Korir amezuru eneo la Masalani ,kaunti ya Garissa kilomita chache na msitu wa Boni ambapo Al shabab wamekuwa wakifanya mashambulizi na kujificha .
-
Utayari wa ukanda wa Afrika kupambana na magonjwa ya milipuko
19/02/2025 Duração: 10minKatika siku za hivi punde magonjwa ya milipuko imeripotiwa katika mataifa ya Afrika ,ikiwemo Ebola Marburg na Mpox
-
Juhudi za Guinea kumaliza ugonjwa wa Malale mojawapo ya magonjwa yaliyotengwa
05/02/2025 Duração: 10minGuinea itakuwa ni taifa la nane la Afrika kuthibitishwa kuangamiza ugonjwa wa malale Guinea imekuwa ilishiriki katika majaribio ya matibabu ya ugonjwa wa malale ambayo yalifanyiwa utafiti mara ya kwanza nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya CongoTimu ya madaktari kutoka DRC na Guinea walishirikishwa kwenye majaribio hayo na kwenye makala haya tumezungumza na Dkt Chirac Bulanga kutoka DRC