Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editora: Podcast
  • Duração: 8:04:24
  • Mais informações

Informações:

Sinopse

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

Episódios

  • Uchaguzi wa Marekani, mapigano DRC, kampeni za Raila kuwania uenyekiti wa tume ya AU

    09/11/2024 Duração: 20min

    Donald Trump achaguliwa kuwa rais wa 47 wa Marekani, Ziara ya rais wa Kenya William Ruto huko Addis Ababa Ethiopia, na Sudan Kusini, na Raila Odinga kuzindua azma yake ya kuwania uenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Februari mwaka 2025. Mapigano makali kati ya waasi wa M23 na wazalendo mashariki mwa DRC, Umoja wa Mataifa wasema uamuzi wa kuahirishwa uchaguzi nchini Sudani Kusini haukubaliki, Duma Boko atawazwa rasmi kama rais mpya wa Botswana, Uhusiano wa Urusi na Marekani baada ya Trump kushinda uchaguzi

  • Kithure Kindiki aapishwa kuwa makamu wa rais Kenya, ziara ya rais wa DRC nchini Uganda

    02/11/2024 Duração: 20min

    Kuapishwa kwa makamu mpya wa rais wa Kenya Profesa Kithure Kindiki, ziara ya rais wa DRC Félix Tshisekedi Kampala Uganda huku mapigano kati ya waasi wa M23 na wazalendo yakiripotiwa mashariki mwa nchi yake, mkutano wa Comesa watamatika Jijini Bujumbura Burundi, Umoja wa mataifa wasema hali ya kibinadamu nchini Sudan yatia wasiwasi, upinzani washinda uchaguzi mkuu Botswana, kampeni za lala salama Marekani, lakini pia kauli ya Korea Kaskazini kuwa itasimama na Urusi hadi ushindi wake huko Ukraine.

  • Rais Tshisekedi asema katiba ya Congo itarekebishwa, kesi ya naibu rais wa Kenya

    26/10/2024 Duração: 20min

    Kauli ya rais wa DRC kuhusu marekebisho ya katiba yazua hisia mseto, kesi ya naibu wa Rais wa Kenya aliyeenguliwa madarakani Rigathi Gachagua yaendelea, umoja wa Ulaya kuendeleza shinikizo ilizoiwekea Burundi mwaka 2015 hadi mwaka 2025. Ziara ya mkuu wa UNHCR Fillipo Grandi nchini Uganda, mgombea wa chama tawala kule Msumbiji awa mshindi wa uchaguzi mkuu, uchaguzi mkuu wa Marekani na mengineyo.

  • Naibu rais wa Kenya Gachagua atimliwa, usalama wa mashariki ya DRC wajadiliwa Luanda

    19/10/2024 Duração: 20min

    Kuondolewa madarakani kwa naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua na uteuzi wa profesa Kithure Kindiki, serikali ya Kinshasa yakaribisha makubaliano yaliyoafikiwa kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa DRC na Rwanda kuhusu suala kulitokomeza kundi la FDLR na Rwanda kusema iko tayari kuwaondoa wanajeshi kwenye ardhi ya Congo, maandamano ya upinzani kule Msumbiji baada ya uchaguzi mkuu, kuuawa kwa kiongozi wa Hamas Yahya Sunwar, uchaguzi mkuu wa Marekani na mengineyo.

página 2 de 2